Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, Katika mkutano wa kumbukizi ya mashujaa wa wanawake wa Gilan, ambao uliandaliwa kama sehemu ya Kongamano la Pili la Mashujaa 8000 wa Mkoa wa Gilan na kuhudhuriwa na familia za mashujaa pamoja na wanaharakati wa masuala ya kitamaduni, washindi wa shindano la kitaifa la kazi za kisanii lenye mwelekeo wa "mashujaa wa wanawake" walitangazwa na kutuzwa rasmi.
Shindano hili lililenga kuwasilisha kwa ubunifu wa kisanii hadithi za kujitolea na mchango mkubwa wa wanawake mashujaa katika historia ya kisasa ya Iran. Mashindano yalifanyika katika fani mbalimbali kama vile: Upigaji picha, uchoraji, podikasti, filamu za makala fupi, uandishi wa kaligrafia, mahojiano, maandishi ya moyoni, ushairi na hadithi fupi.
Miongoni mwa washindi wa shindano hili ni:
-
Tahereh Rezaei kutoka Rustamabad katika kipengele cha upigaji picha
-
Forough Faraji kutoka Rudbar katika uchoraji kwa kalamu nyeusi
-
Alireza Mirzazadeh kutoka Rudsar katika podikasti
-
Fatemeh Mahdizadeh kutoka Rasht katika filamu ya makala fupi
-
Hengameh Mohammaddokht kutoka Rasht katika kaligrafia
-
Homa Akbari katika kipengele cha mahojiano
-
Kobra Mohammadi kutoka Astaneh Ashrafiyeh katika kipengele cha ekolayza (visual audio art)
-
Zahra Babaei kutoka Amol katika maandishi ya moyoni (delneveshteh)
-
Sara Shojaei kutoka Yasuj katika hadithi fupi
-
Sara Ramazani katika ushairi, na
-
Sousan Hajipour kutoka Shiraz katika kaligrafia ya kisanii
Katika hafla hiyo, si tu kazi bora zilitangazwa, bali pia kina mama na familia za mashujaa waliheshimiwa kwa kupewa vyeti vya kutambua mchango wao pamoja na maua kama ishara ya heshima na shukrani.
Your Comment